KITUO CHA AFYA HEDARU CHAANZA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI
Kituo cha afya cha Hedaru kilichopo halmashauri ya wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro mapema tarehe 4/9/2023 kimeanza rasimi kutoa huduma za upasuaji mkubwa baada ya kukamilika kwa uwekwaji wa vifaa tiba vya kisasa.
Katika operesheni ya kwanza iliyofanikiwa vizuri,mtoto aliyepatikana aliyepewa jina la Samia amezaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.5.kufanyika kwa operesheni hiyo ni utekelezwaji wa maagizo yaliyotolewa na timu ya usimamizi na ushirikishaji kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI yaliyoelekeza kuanza mara moja kwa zoezi hilo baada ya ukamilishwaji wa jengo na uwekwaji wa vifaa tiba katika kituo hicho cha afya.

Comments
Post a Comment