TAASISI YA MIFUPA (MOI)IMETOA UFAFANUZI KUHUSU VIDEO YA KUKISS ILIOSAMBAA MITANDAONI ,MHUSIKA AOMBA RADHI.
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili uliofanywa na Mgonjwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa Mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023 ambapo katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na Mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.
“Menejimenti imebaini kwamba Mpenzi wa Mgonjwa huyo si Mtumishi wa Taasisi ya MOl, aidha tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia Wahusika kuendelea na kitendo hicho, Menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa Wahusika”
“Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna Mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video, Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na Mgonjwa huyo pamoja na Mpenzi wake, vilevile Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na Mgonjwa jirani”.
Kutokana na kuwepo kwa hali ya sintofahamu iliyojitokeza baada ya video moja iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kumuonyesha mgonjwa mmoja akifanya tendo la busu la midomo na ndimi na mwanamke mmoja ambaye hapo awali alitajwa kuwa ni mmoja wa wahudumu wa hospitali hiyo lakini uchunguzi baadaye ulionyesha kuwa mwanamke huyo ni mpenzi wa mgonjwa huyo.
Kufuatia Uchunguzi huo uliofanyika, hatimaye mgonjwa huyo amekiri kufanya tendo hilo huku akiomba msamaha kwa jamii yote ya watanzania pamoja na taasisi ya mifupa MOI kutokana na kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili alichokifanya akiwa na mpenzi wake Hospitalini hapo huku akiahidi kwamba hatorudia tena kufanya kitendo kama hicho ambacho ambacho kilizua hali ya taaruki miongoni mwa watanzania pamoja na Taasisi ya MOI kwa ujumla wake.
Aidha, Taasisi ya MOl inaendelea kuwakumbusha wagonjwa pamoja na ndugu wa wagonjwa kuheshimu miongozo ya Wizara ya Afya kwa kutofanya vitendo vyenye uvunjifu wa maadili au kupiga picha/video katika maeneo ya kutolea huduma za afya.
#EthanmediaUpdates.

Comments
Post a Comment