SIMBA SC NA SAKHO


 SAKHO NA SIMBA MAMBO MAGUMU


Winga machachari, Pape Ousmane Sakho ameomba kusepa kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. Inaelezwa, Sakho amepata ofa kutoka Ubelgiji na Ufaransa, lakini bado ana mkataba na Simba hivyo memejimenti ya mchezaji huyo imeuandikia uongozi wa Msimbazi kuomba imruhusu kuvunja mkataba ili adili na ofa alizonazo. 

.

Sakho amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja inadaiwa ana ofa kutoka Stade Malherbe Caen na Grenoble zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Ufaransa, lakini ikielezwa kuna klabu ya Ubelgiji nayo inamtaka. Sakho amepata ofa hizo baada ya mfululizo wa kiwango bora ikiwamo kuitwa Timu ya Taifa ya Senegal pamoja na tuzo yake ya Bao Bora la CAF. Hadi sasa Sakho yupo zake kwao Senegal akisubiri hatma yake. 

.

Kama Simba itashindwa kumuachia Sakho katika kipindi hiki, staa huyo atarejea kikosini, lakini hataongeza mkataba na atacheza hadi msimu umalizike kisha aondoke akiwa mchezaji huru.

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI