MASHINE KUTUA SIMBA


 Habari njema kwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya SIMBA ni kunaswa kwa saini ya winga wa maana anayejua kazi na mbio mithiri zenye hatari kutoka Asec Mimosas, KRAMO AUBIN 🇨🇮 

.

Fundi Kramo msimu uliopita kwenye mechi za makundi ya Kombe la Shirikisho aliupiga mwingi na kufunga mabao manne na assist tatu katika mechi tatu kati ya sita za hatua hiyo na timu hiyo kutolewa nusu fainali na USM Alger iliyobeba ndoo mbele ya Yanga.

.

Mabosi wa Simba wamefanikiwa kunasa saini yake baada ya kupambana kwelikweli na watani wao Yanga pia staa huyo alikuwa na ofa kutoka Morocco.

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI