BREAKING NEWS
🚨BREAKING NEWS!
Majadiliano ya muda mrefu baina ya uongozi wa @yangasc na Fiston Kalala Mayele yamefikia tamati kwa mshambuliaji huyo kuuambia uongozi kuwa anahitaji kupata changamoto mpya.
Fiston alibakisha mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara.
🎯 kutoka kwenye chanzo cha kuaminika Fiston Kalala Mayele atakua mshambuliaji mpya wa klabu ya @pyramidsfc ya nchini Misri.
BIASHARA:
Biashara ya kwanza ya team ni kuuza wachezaji, Yanga imevuna kiasi cha takribani 2B kwenye uhamisho wa mshambuliaji wao nyota. Pongezi kwa klabu na uongozi kwa ujumla kwa kufanya maamuzi ya kimpira na kuingizia klabu kiasi cha pesa kitakacho fanikisha ujenzi mpya wa kikosi na miundombinu ya klabu.
Kamanda @mayelefiston kila la kheri..

Comments
Post a Comment