UPDATE YA NABI
NABI APEWA SAA 48 KAIZER CHIEFS
.
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi πΉπ³ amesema ndani ya saa 48 mustakabali wake na Kaizer Chiefs utakuwa umejulikana.
.
Kaizer Chiefs πΏπ¦ imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamtaka kocha huyo, lakini jana akihojiwa na The South African alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 watakuwa wameshamalizana.
.
“Kwa sasa ni ngumu kukupa taarifa, lakini tambua kuwa tunaendelea kuzungumza na viongozi wa Chiefs kupitia wakala wangu na ndani ya saa 48 tutakuwa tumeshakamilisha na kufahamu nini kinaendelea,” alisema.

Comments
Post a Comment