NESTORY IRANKUNDA UPDATE
Kwa majina anaitwa Nestory Irankunda,alizaliwa Tarehe 9 Feb 2006 Katika Kambi ya Wakimbizi Kasulu Mkoani Kigoma, Tanzania 🇹🇿 kutoka katika Wazazi Wenye asili ya Burundi 🇧🇮
Irankunda anatajwa kuwa yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na Timu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea katika klabu yake ya Adelaide United ya Australia na mpaka sasa ameshachezea timu ya vijana Australia pia aliitwa mara Moja katika timu ya wakubwa lakina hakutumika
Nmemfatilia kwa kiasi flani ni Moja ya talent nzuri sana akiwa na umri Miaka (17) tu anakichafua balaa katika ligi kuu ya Australia kwa kiwango Cha juu ni winga,na katika sehemu mbalimbali zinazohusu Upcoming/scout report,jina lake lipo,
Bado Kijana Huyu ananafasi Kubwa sana ya kuchagua kuwakilisha Kucheza Timu ya Taifa ya TANZANIA ama Burundi inategemea na ushawishi japo nafasi hiyo ni ndogo sana hua ni ngumu kukataa kuchezea mataifa ya mbele kwa Hawa ndugu zetu..mwenye kujua story yake zaidi huyu kijana?
Tanzania Kwa sasa imeruhusu Wanamichezo Wenye Asili ya Tanzania ambao wapo Nje Kurudi Kucheza Katika Timu za Taifa na watatambuliwa Kwa Vibali maalumu kama Watanzania Hata kama Bado ni raia wa Nchi Husika Hivyo Kuna Haja ya TFF na Vyama vingine vya Michezo Kuendelea kutafuta Vipaji kama Hivi Vilivyopo Nje kuja Kutumikia Timu yetu ya Taifa, Ni Muda wa kuachana kutegemea Wachezaji kutoka Simba na Yanga Pekee hasa kwenye Soka Vipaji vipo vingi Nje

Comments
Post a Comment