MGUNDA UPDATE
🚨 JUMA MGUNDA UPDATE
Wakati jitihada za kujiweka sawa na msimu ujao zikiendelea inasemekana kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC Robertinho Oliviera anataka kulisuka upya bench lake la ufundi kuanzia kocha wa makipa, kocha wa viungo pamoja na msaidizi wake namba moja.
Kuna miamba ambayo Robertinho amependekeza kuongezewa katika Bench la ufundi na hivyo kusababisha karibu Bench zima la ufundi kupewa mkono wa kwaheri.
Jinamizi lipo kwa Kocha Juma Ramadhan Mgunda ambae anatakiwa kuchukua mikoba ya kuinoa Simba Queens. Hata hivyo Mgunda amekataa ofa hiyo na kuuomba uongozi wa Simba kuwa endapo wameona kuwa hafai kuendelea kukaa Katika Bench la Simba SC basi wamalizane nae atafute maisha yake sehemu nyengine.
#sportsnewsappdate💪

Comments
Post a Comment