MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA MIZIGO TANZANIA
HABARI PICHA
Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL ikiwasili na kumwagiwa maji watersalute mara baada ya kutua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi wenginewakati akikata utepe kuzindua Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Juni, 2023.
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa kwenye Chumba cha Marubani ya Ndege mpya ya Mizigo aina ya Boeing 767-300F ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL mara baada ya kuizindua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es Salaam




Comments
Post a Comment