LYANGA TO JKT
🚨 JKT YAMREJESHA LYANGA
.
JKT Tanzania inaendelea kujipanga kwa msimu ujao wa Ligi Kuu baada ya kupanda sambamba na Kitayosce kwa kufanya usajili wa kimya kimya na safari hii imemrejesha kikosini nyota wake wa zamani, Danny Lyanga aliyekuwa akikipiga Geita Gold akiwa pia nahodha wa timu hiyo.
.
Lyanga aliyewahi kuwika na Coastal Union, Simba na Azam, amesainishwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa ni kati ya wachezaji wapya waliokuwa wakipigiwa hesabu na benchi la ufundi la JKT. Wengine waliotua JKT yupo Aziz Kader aliyeachwa na Azam FC na Deusdedit Okoyo.

Comments
Post a Comment