LUIS JOSSEE MIQUISSON UPDATE:
Simba mapema waliamua kumshirikisha Robertinho juu ya hatua hiyo na kiwango cha winga huyo ambapo Mbrazil huyo aliwaambia mabosi wake; 'Nileteeni mtu wa kazi huyo.'
"Mshahara huo anaoutaka ni mkubwa kwa klabu zetu hapa, ingawa tunaheshimu na kutamani sana arudi lakini bado tunapambana naye kuangalia kama atarudi chini na kutusikiliza," kilisema chanzo makini kutoka ndani ya Simba.
Mtihani mwingine wa Simba ni jinsi gani itamalizana na Al Ahly inayohitaji kiasi kisichopungua Dola 250,000 (Sh592 milioni) ili wamuachie Luis ambaye bado ana mkataba na Waarabu hao.Kwa sasa Luis hayupo kwenye hesabu za Al Ahly kwa msimu huu na tayari kocha wao Marcel Koller raia wa Uswisi ameshindwa kukubaliana kiwango cha winga huyo.
Hata hivyo, upande mwingine Simba inapiga hesabu kuwa kama watashindwana na Luis basi irudi sokoni kuangalia chaguo lao la pili kufanikisha usajili wa kushusha winga mwenye kasi, huku Kramo Aubin wa Asec Mimosas ya Ivory Coast na Makabi Lilepo wa Al Hilal ya Sudan wakitajwa.

Comments
Post a Comment