JOASH ONYANGI UPDATES.
Beki wa kati wa klabu ya Simba SC, Joash Onyango ameandika barua ya pili kwenda kwa uongozi wa klabu ya Simba akiomba kuondoka ndani ya klabu hiyo kutokana na kutokuwa na furaha. Onyango mwenye umri wa miaka 30 ameutaka uongozi wa Simba umuachie huru kwani hana amani tena ya kuendelea kucheza Simba.
Uongozi wa klabu hiyo unaendelea kujadiliana kuhusu hatma ya beki huyo aliyebakiza mkataba wa mwaka mmoja. Simba wanataka kumpata mbadala sahihi wa Onyango ndio wampe mkono wa kheri (Thank You) na wanahaha kutafuta saini ya beki wa klabu ya Cotton Sports ya Cameroon, Che Fondoh Malone.
#sportsnewsupdates💪

Comments
Post a Comment