AMESUSA !!!!!!
Rais wa Yanga Engineer Hersi Saidi amesusia kikao cha Uongozi ndani ya klabu hiyo ambacho kilikaa siku ya jumamosi kujadili hali inayoendelea katika timu hiyo na namna ambavyo wanaweza kupata mibadala ya wachezaji wanaoondoka ndani ya kikosi hicho.
Kikao hicho pia kilijadili namna gani wataweza kumalizana na wachezaji wa Yanga Princess ambao wanaidai Yanga malipo yao ya mishahara ya malimbikizo pamoja na pesa za usajili kisha wakajadiri ni kwa namna gani wanaweza kupata wachezaji mbadala na kocha mwenye uwezo kama Nabi ambaye ameondoka zake.
Mara baada ya uchangiaji wa mada juu ya agenda hizo ndio mjumbe mmoja akashindwa kujizuia kwa kumwambia Rais huyo kuwa yeye ndio amekuwa chanzo cha wachezaji wazuri na makocha wao kuondoka hivyo anapaswa kujirekebisha mara baada ya kusema hivyo kiongozi huyo kutokaa Salamander tower alihamaki akakasirika sana na kuamua kuondoka ndani ya ukumbi wa mikutano wa hotel hiyo ya kifahari Serena iliyopo jijini Dar es salaam.
Mara baada ya Rais huyo kuondoka kikao kikavurugika wajumbe wengine wakashindwa kuendelea na kikao hicho ambacho pia kilitakiwa kujadili hatima ya mkutano mkuu wa Yanga unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni

Comments
Post a Comment