ZIMBWE APEWA MKATABA MPYA DONGE NONO .
Katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, mabosi wa Simba wameamua kumzuia beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa kumwekewa Sh 300 milioni mezani ili asiende Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini iliyokuwa inammnyemelea ili imsajili.
.
Ipo hivi. Tshabalala amebakiza mechi mbili tu kuuaga msimu huu na kumalisha mkataba wa alionao kwa sasa, lakini ni mmoja wa mabeki ambao Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ anayetaka kuona anasalia kikosini na fasta mabosi wa klabu hio wamempa mkataba mpya wenye dau nono.
.
Nahodha huyo msaidizi aliwapa kazi ngumu mabosi wa timu hiyo kumbakiza Msimbazi kutokana na ofa kubwa aliyokuwa amepewa na Kaizer Chiefs iliyowekwa dau la Sh 200 milioni na mshahara wa Sh 20 milioni kwa mwezi, lakini walipambana na kumalizana na beki huyo kusaini dili jipya.
.
Inaelezwa Simba ilishtuka mapema baada ya taarifa za kutakiwa kwa Tshabalala na kuamua kukaa naye mezani na kupata mwafaka katika majadiliano ya muda mrefu chini ya menejimenti yake na hatimaye akakubali kusaini dili hilo la miaka mitatu kwa kupewa Sh 300 milioni na mshahara wa Sh 10 milioni.

Comments
Post a Comment