YANGA WAPEWA REFA WA NUKSI



.

Mwamuzi mwenye bahati mbaya na timu zinazocheza ugenini, Ibrahim Mutaz wa Libya 🇱🇾 amepangwa kuchezesha mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Marumo Gallants na Yanga itakayochezwa kesho Jumatano

.

Mutaz amechezesha mechi 11 za mashindano ya klabu Afrika ambapo kati ya hizo, timu zilizokuwa nyumbani zilipata ushindi mara 10 na mara moja iliobakia, mechi ilimalizika kwa sare.

.

Ni refa asiyependa mzaha kwa wachezaji wanaocheza rafu na watovu wa nidhamu kwani katika mechi hizo 11, ametoa kadi 57 ikiwa ni wastani wa angalau kadi tano kwa mchezo, kati ya hizo, kadi 54 ni za njano na kadi nyekundu tatu.

.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepanga Mutaz asaidiwe na Mlibya mwenzake Attia Essa Amsaad na Mtunisia.

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI