WAARABU WANAMTAKA ROBERTINHO

 

WAARABU WAMSAKA ROBERTINHO

.

Simba imeacha gumzo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ni ubora wao uwanjani na sasa kama kuna mtu anayesakwa ni kocha wao Robert Olivieira ‘Robertinho’.

.

Mezani kwa Robertinho ofa mbili kubwa ambazo inategemea na akili kubwa ya mabosi wa Simba na uamuzi wa kocha huyo raia wa Brazil. Tuanze na Misri klabu ya Al Ittihad, inayoshiriki ligi kuu nchini humo imempigia simu kocha huyo ikitaka huduma yake baada ya kuona hesabu zao za kuingia ndani ya klabu tatu za juu kuwa na mashaka.

.

Al Ittihad sasa inafundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Zolan Maki ambaye kabla ya kutua huko alitokea hapa nchini wakiona bado hawajakubali mwendo wa kocha wao huyo raia wa Serbia. Katika mechi zao tano za mwisho Al Ittihad imeshinda mechi moja na kupoteza tatu huku wakitoa sare moja hatua ambayo imewatisha mabosi wa klabu hiyo wakianza mchakato wa siri.

.

Akizungumzia jana kwa kifupi Robertinho licha ya kukiri ofa kuwa nyingi kwake alisema kwa sasa anataka kuitumika Simba kuhakikisha anatengeneza timu tishio Afrika.


…………


@tonsimbasportsclub

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI