UKIMUELEWA DI CANIO HUWEZI KUMUELEWA CHAMA, UKIMUELEWA ZIDANE UTAMUELEWA CHAMA .
.
Euro 2020 pale Romania kwenye dimba la National Arena, Bucharest beki wa Ujerumani Antonio Ruddiger alimnyata mgongo kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, lakini mpira ulivyoisha alienda kumuomba radhi!! Yes ulikuwa ni uungwana tu, Pogba akuumia kiasi cha kushindwa kuendelea kucheza ila Ruddiger aliamua kukumbuka FOOTBALL IS FAIR PLAY.
.
Uefa Champions League 2015 kule Uholanzi, dunia ilishuhudia rafu mbaya kwenye soka baada ya Hector Moreno wa PSV kupiga brashi kali mpaka mguu wa beki wa Utd Luke Shaw ukavunjika!! Lakini alimfuata palepale uwanjani na kumpa pole ila inasemekana pia alifika mpaka hospitali kumtembelea mchezaji mwenzake!! Yes ni uungwana tu.
.
Msimu huu pia tulishuhudia FAIR PLAY nyingine baada ya beki wa Southampton Kyle Walker Peters kumuumiza kinda Allejandro Garnacho, alimtumia ujumbe wa pole na kumtaka radhi lakini hii FAIR PLAY sio sheria ni ubinadamu tu ambao mtu anakuwa nao.
.
Mwaka 2006 kwenye fainali ya World Cup kule Ujerumani Zinadine Zidane alimpiga kichwa Marco Matterazi wa Italia ila wanadai wakati mchezo unaendelea Zizzou alimwambia Marco asiivutevute jezi yake mpira ukiisha atampatia, kwa jeuri Matterazi akamjibu hataki hio jezi bali anamtaka dadaake Zidane 😃, kilipigwa kichwa kizito na sikumbuki kama kuna FAIR PLAY iliyotolewa.
.

Comments
Post a Comment