UGANDA, MUSEVENI ASAINI KUPINGA USHOGA
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini moja ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya Watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga, Spika wa Bunge Anita Among ametangaza mapema hii leo na kupuuzia vitisho na hatari za vikwazo kutoka kwa Wafadhili kutokea Nchi za Magharibi.
Mahusiano ya Watu wa jinsia moja tayari yalikuwa yamepigwa marufuku nchini Uganda huku marufuku hiyo ikiwa katika zaidi ya Nchi 30 za Afrika lakini sheria hiyo mpya inakwenda mbali zaidi katika kuwalenga Wasagaji, Mashoga, Watu wa jinsia mbili na Watu waliobadilisha jinsia zao ikitoa hukumu ya kifo kwa kile kinachoitwa ushoga uliokithiri, ambayo ni pamoja na kufanya mapenzi ya jinsia moja wakati Mtu ana maambukizi ya UKIMWI na kifungo cha miaka 20 kwa kusambaza na kuhamasisha ushoga.
Utiaji saini wa muswada huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza na Spika wa Bunge la Uganda Anita Among kupitia ukurasa wake wa Twitter huku Mamlaka zikikiri kuwa Uganda ambayo inapokea mabilioni ya dola kama msaada wa kigeni kila mwaka, inaweza kukabiliwa na vikwazo kutokana na sheria hiyo.
Itakumbukwa Museveni alipotia saini sheria yenye vizuizi kidogo dhidi ya ushoga mwaka 2014, Serikali za Magharibi zilisitisha baadhi ya misaada huku ikiwekea vikwazo vibali vya kusafiria (visa) na kupunguza ushirikiano wa kiusalama, Muungano wa Kampuni za Kimataifa , ikiwemo Kampuni ya Teknolojia ya Marekni ya Google ulikosoa sheria hiyo na kuonya kuwa itaweka wale wanaofanya kazi nchini Uganda katika hali ngumu na kuumiza uchumi wa nchi.
.jpeg)
Comments
Post a Comment