SHABIKI WA SIMBA AKUTANA NA C.E.O NA KUMPA KERO ZAKE

 






Wiki mbili zilizopita nilikwenda kukutana na mtendaji mkuu wa club yetu ya Simba nikiwa na hoja au Mambo 5 ambayo nilikwenda kuzungumza na CEO wetu ni haya yafuatayo .


1.USAJILI


Kuhusu maboresho ya kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao akakiri kuwa kuna mapungufu yapo wao kama uongozi wameyaona na watafanya usajili mzuri sana.


2.JEZI ZA MSIMU MPYA


wamekiri kuwepo na Tafrani ya kuchelewa kwa jezi za msimu mpya lakini msimu huu hilo jambo halitojitokeza tena 


3.KADI ZA WANACHAMA


wanashughulikia mfumo wa kidigital wa wanachama wapya na 

soon watatoa utaratibu mzuri kwa wanachama kujisajiri


4.TAMASHA LA SIMBA DAY


Hoja yangu ilikuwa tamasha la Simba day linapaswa kuboreshwa zaidi ya hivi lilovyozoeleka ili lilete mvuto zaidi tofauti na hapo nyuma


5.DIGITAL PLATFORM ZA SIMBA


Hoja yangu ilikuwa idara hiyo iongezewe watu wa kufanya kazi na kupush maudhui ili digital platforms za club zichangamke zaidi 


Mara baadaya ya uwasilishaji wa hoja zangu hizo alinihakikishia kuwa yote hayo yataboreshwa na kufanyiwa kazi kwa kiwango cha hali ya juu kuhakikisha timu yetu inakuwa bora zaidi msimu ujao na hatimaye kuchukua makombe yote ya ndani ligi kuu, Fa na kufika mbali ligi ya mabingwa Barani Africa. 


Kwahiyo wana Simba wenzangu tuwe na subira na tuwaamini viongozi wetu kuna mazuri yanakuja mbeleni

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI