SAMATTA ABAKIZA MOJA UBINGWA



Michezo ya raundi ya mwisho kwenye mchujo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji wikiendi ijayo ndio iliyobeba matumaini ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta kutwaa ubingwa wake wa pili akiwa na KRC Genk.

.

Timu hiyo ipo katika nafasi ya tatu kwenye mchujo huo wa ubingwa huku ikiwa na pointi 45 ipo nyuma kwa tofauti ya pointi moja iliyoachwa na Union Saint-Gilloise inayoongoza na alama 46, ikifuatiwa na Royal Antwerp inayolinagana nayo pointi (46) zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

.

Katika michezo yote kuelekea wa mwisho, Samatta amekuwa akikiwasha kikosi cha kwanza na mchango wake katika kutoa pasi za mabao unaonekana.

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI