RIPORT YA ROBERTINHO
-Ripoti ya kocha mkuu wa klabu ya Simba SC, Roberto Oliveira kwa bodi ya wakurungezi wa klabu hiyo inataka usajili wa wachezaji 8 wapya ikiwa wachezaji 5 wa kimataifa na wachezaji 3 wawe wachezaji wa ndani. Katika ripoti hiyo Robertinho anataka golikipa, Beki wa kushoto, Beki wa kati, Viungo wawili, Winga mmoja na washumbuliaji wawili
-Katika mapendekezo yake kocha anataka wachezaji watano wapya wa kimataifa (Golikipa, Beki wa kati, Kiungo wa kati, Winga na mshambuliaji mmoja) huku akihitaji wachezaji watatu wa ndani (Beki wa kushoto, Kiungo wa kati na Mshambuliaji mmoja) kwenye ripoti hiyo kocha anataka wachezaji wanaocheza timu zao za taifa na wawe kwenye kikosi cha kwanza kwenye timu wanazotoka.
-Pia kocha huyo amependekeza kuachana na wachezaji Mohamed Ouattara, Agustine Okrah, Peter Banda, Ismail Sawadogo, Gadiel Michael, Beno Kakolanya na Habibu Kyombo ila Banda ameomba aondoke kwa mkopo na ameomba wachezaji wawili wa kimataifa Pape Sakho na Joash Onyango wasiondoke Simba kwa sasa kwani wachezaji hao wameomba kuondoka.
-Wachezaji wa kimataifa wenye uhakika wa kuendelea kubaki Simba kwa msimu ujao 2023/24 ni Beki Henock Inonga Baka, Viungo Sadio Kanoute, Clatous Chama na Sadio Ntiazonkiza na washambiaji Moses Phiri na Jean Baleke pamoja na hayo kocha ameomba kuongezewa watu kwenye bechi la ufundi ili kuifanya Simba kuwa tishio zaidi ya msimu huu.

Comments
Post a Comment