NABI AWAFANYIA USHUSHUSHU WAARABU .
.
Kama unafikiri Yanga itaingia kizembe kwenye mechi mbili za fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, SAHAU kwani tayari kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ametuma makachero kuwasoma wapinzani wao USM Alger na kuwataka wamletee ripoti kamili haraka iwezekanavyo.
.
Makachero hao sio wale wa Usalama 😃 bali ni wataalamu wa soka ambao kazi yao ni kuwasoma wapinzani, kutathimini kikosi chao, ubora wao, Wachezaji wa kuchungwa, aina yao ya kucheza wakiwa na mpira na hata wasipokuwa na mpira.
.
Nabi alifanya hivyo juzi usiku baada ya kumalizika kwa mechi ya USM Alger na Asec Mimosas na kujua atakutana fainali na Alger.
.
Benchi la Yanga linaamini ili kupata haraka mikanda ya mechi za Alger na tathmini fupi ya timu hiyo linatakiwa pia kutafuta Wataalamu kutoka Alger wanaoijua vyema timu hiyo ili kupata kiuhalisi mafaili wanaoyahitaji kisha kutaweka mezani kuyaundia mpango mkakati jambo ambalo hadi sasa linaenda vizuri.

Comments
Post a Comment