MAREKEBISHO MENGINE KUHUSU MKAPA STADIUM







 CAF KUHUSU SEHEMU YA KUCHEZEA (PITCH)

.

Kamati ya CAF imeshauri sehemu ya kuchezea kuwa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ya CAF Super League na inatakiwa kufanyiwa marekibisho makubwa na kuweka (hybrid pitch). Hizi ni nyasi asilia lakini zikiwa na mchanganyiko kidogo wa nyasi bandia.

.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinaonyesha uwekaji wa nyasi hizo ni wa haraka na unaweza kutumia kati ya siku sita hadi saba. Hata hivyo, inaonekana ni nyasi bora kabisa kwa maendeleo ya soka kwani zina uwezo mkubwa kulinda afya za wachezaji wanaozitumia, zinawafanya kuwa na ari ya kujiamini lakini kukimbia kwa kasi zaidi na vilevile zikiwafanya wachezaji kuwa na ubora wao kwa muda mrefu.

.

Taarifa inaonyesha ni nyasi ambazo zinaweza kudumu kwa miaka nane hadi 10 bila kubadilishwa, lakini ikisema lazima taratibu zote zinazotakiwa kwenye nyasi hizo zifuatwe ikiwemo matundu maalumu ya kupitisha hewa na maji uwanjani yawepo.

.

Pia, kamati hiyo imesema mitambo ya umwagiliaji maji inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kila sehemu inapata maji ya kutosha kulingana na viwango. Kamati hiyo imesema eneo hili linatakiwa kukamilika Agosti 1, 2023.

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI