KIWEPESI MANCHESTER CITY
.
Arsenal ilitema rasmi ubingwa kwa msimu huu baada ya kukubali kichapo cha mabao 1-0 kutoka kwa Nottinghm Forest na kuiwezesha Man City kuchukua ubingwa ikiwa sebuleni.
.
Huu unakuwa ni Ubingwa wa tatu mfululizo kwa Manchester city na hiyo imeifanya kuweka rekodi ya kuwa timu ya tano tu kufanya hivyo ikiungana na Huddersfield Town, Arsenal, Liverpool na Manchester United.
.
Mbali ya Arsenal kupoteza ubingwa pia imepoteza kiasi kikubwa cha pesa ambacho ingekipata kama ingekuwa bingwa. Kiasi hicho cha pesa kinatokana na zawadi ya bingwa ambayo msimu uliopita Man City ilipokea Pauni 161 milioni (Sh 474 bilioni) ambayo ni mjumuisho wa zawadi zote ikiwa pamoja na pesa ya haki ya matangazo ya televisheni.

Comments
Post a Comment