IJUE HISTORIA YA BERNARD MEMBE




KONA YA HISTORIA; HUYU NDIE BERNARD MEMBE


KUZALIWA


BERNAD MEMBE alizaliwa Novemba 9, 1953, Rondo, Chiponda, katika Mkoa wa Lindi, akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto saba (7) waliozaliwa katika familia ya Mzee Kamillius Anthony Ntachile na Mama Cecilia John Membe.


Elimu:


1962 – 1968: Elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Chiponda, Lindi.


1969 – 1972: Elimu ya Sekondari, (O-level) Namupa Seminary, Lindi


1973 – 1974: Kidato cha tano na sita (A-level) Itaga Seminary, Tabora


1975 – 1980: Aliajiriwa serikalini, ofisi ya rais.


1981 – 1984: Alipata Shahada ya kwanza katika tasnia ya Sayansi katika masuala ya Siasa na mahusiano ya kimataifa.


1985 – 1989: Aliendelea na ajira yake serikalini katika katika ofisi ya rais


1990 – 1992: Alipata Stashada ya Uchumi, Mahusiano ya Kimataifa na Sheria za Kimataifa


1993 – 1994: Alirudi serikalini kuendelea na kazi kama mchambuzi za mambo ya ulinzi na usalama


Mafunzo.. 


Kati ya mwaka 1975 na 1976 Bernard Membe alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, Arusha.


Mwaka 1978, Ndugu Membe alipata Mafunzo ya sheria za Jinai na usalama wa nchi, nchini Uingereza.


Mwaka 1980, Ndugu Bernad Membe alipata mafunzo ya siasa, katika Chuo cha Chama cha Mapinduzi (CCM), Kivukoni, Dar es Salaam, ambacho sasa ni Chuo cha Mwalimu Nyerere.


UTUMISHI KWA KIFUPI


2006 – 2020: Mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


2008 – Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Africa, Addis Ababa, Ethiopia.


Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kutoka muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini, SADC


2006 – 2011: Katibu wa Secretariat ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, CCM.


2006 – 2011: Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.


2006 – 2020: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Taifa


2013 – 2020: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Madola Commonwealth


2014 – 2020: Mwenyekiti Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI