FEI TOTO ASHITAKIWA
FEITOTO ASHITAKIWA KAMATI YA NIDHAMU NA YANGA.
Uongozi wa klabu bingwa ya soka Tanzania Bara ya YANGA SC @yangasc umemshitaki kwa Kamati ya nidhamu ya klabu mchezaji wake FEISAL SALUM ABDALLAH kwa makosa ya utovu wa nidhamu.
Wakati huo huo habari zinasema kwamba upande wa mchezaji umeamua kuwasilisha malalamiko yake CAS (Court of Arbitration in Sports) na huenda leo wakapeleka taarifa kwa klabu (Yanga) kuhusiana na dhamira yao hiyo.
Hii imekuja baada ya Feisal kushindwa kupata anachoamini ni haki kutokana na maamuzi ya kuvunja mkataba na klabu yake. Wakati klabu ikiamini Feisal ni mali yao kutokana na ushindi waliopata kutoka kwenye Kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji, mchezaji yeye ana amini mkataba unampa nafasi ya kuuvunja wakati wowote na kulipia fidia kama kifungu cha 17.4 cha mkataba kinavyosema.
BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)


Comments
Post a Comment