CHANZO CHA MGOMO SOKO LA KARIAKOO
Yapo mambo yaliyoanza kulalamikiwa miaka mingi, na miaka inavyokwenda ndivyo malalamiko yanavyozidi kuongezeka. Yapo yanayoshughulikiwa na Serikali na yapo yanayoonekana kusimika mizizi.
wanacholalamikia wafanyabiashara wa soko hili ni usajili wa stoo zao za mizigo wasioutaka, tuhuma za rushwa kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wasio waaminifu, kamatakamata na kunyanyaswa na kikosi kazi ‘Task Force’ cha TRA, viwango vikubwa vya makadirio ya kodi na utitiri wa kodi.
Haya si mageni, yako Kariakoo, na yako nchi nzima yanayofanyika kwa namna tofauti.
Msingi wa malalamiko yote na mambo yote unaegemea kwenye ‘kukamuliwa’ mapato yao na hofu yao ya kufa kimitaji kutokana na kile kinachodaiwa na wakusanya kodi na ushuru ukilinganisha na kile wanachokiingiza.
.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment