VUNJA BEI MAMBO SIYO MAZURI
⚠️- Taarifa za ndani kutoka kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Duniani @pumafootball kupitia tawi lao la Afrika Kusini @pumasouthafrica wamejiandaa kuwasilisha ofa yao ndani ya Simba SC kwaajili ya kuwa mtengenezaji na msambazaji wa jezi za Simba SC kuanzia msimu ujao.
⚠️Ofa ya Puma inakuja baada ya kuona Simba SC ikifanikiwa kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa kwa miaka ya hivi karibuni na pia baada ya kupata taarifa kwamba timu hiyo itashiriki katika Mashindano ya African Super League kama moja ya Timu 8 za mwanzo.
⚠️Mkataba wa sasa wa Simba SC na kampuni ya Vunja Bei umefika tamati na hakuna mazungumzo yoyote mapya juu ya kuongeza mkataba mpya hivyo hali hiyo inatoa upenyo wa kampuni nyengine kuomba tenda hiyo ifikapo mwishoni mwa Msimu huu.
⚠️Ikumbukwe Puma pia ndio watengenezaji wa jezi za Timu ya Taifa la Senegal, Morroco pamoja na Klabu ya Mamelodi Sundowns.
NB: Wadau wa soka mnasemaje?

Comments
Post a Comment