VITA YA MBINU

 

.

Silaha kubwa ya Nasreddine Nabi ni umiliki wa mpira hasa katikati mwa uwanja kwa pasi za taratibu ambazo hupelekwa pembezoni mwa uwanja kwa mawinga au mabeki wa kushoto na kulia ambao huwa na jukumu la kupiga krosi au pasi za mwisho kwenda kwa washambuliaji.

.

Msanifu wa mbinu hiyo ya Nabi ni kiungo Khalid Aucho ambaye amekuwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi sahihi kwenda kwa wahusika ambao mara nyingi huwa ni winga Ducapel Moloko au beki wa kushoto, Joyce Lomalisa.

.

Hata hivyo Yanga wanapaswa kuwa makini sana na mbinu ya Rivers United kukaba kuanzia katika mstari wa mbele kwani wanaweza kujikuta wakifanya makosa yanayoweza kuwapa faida wapinzani wao ambao ndio wamekuwa wakiitumia kuwanyima uhuru walinzi wa timu pinzani kumiliki mpira na kuanza kujenga mashambulizi.


…………..


Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI