UKIPATA NAFASI TUMIA


 Ukipata nafasi ya kuweka mpira kwenye nyavu tumia , kama ukishindwa kutumia nafasi vizuri basi unaweza ukawa hatarini kushinda mchezo wa mpira wa miguu ndicho kulichowatokea Chelsea pale Stamford.


Chelsea walianza vizuri kwenye shape ya 3-5-1-1 wasipokuwa na mpira wanabadilika wanakuwa na wachezaji wengi wenye uwezo wa kuzuia 5-4-1 How? (Chelsea wakitengeneza mashambulizi mda mwingi Silva anakuwa nyuma then Chalobah na Fofana wanasogea sawa na Enzo & Kova dhumuni ni kufanikisha kuipita pressing ya Madrid + mawingbacks wanakuwa juu zaidi sawa na Kai ambaye nyuma yake kulikuwa na namba 10 wawili Kivip?…


Wakati Chelsea wakiwa wanashambulia Conor na Kante wanasogea juu , kazi yao kubwa ni kushambulia nafasi kati ya CBs na Fbs wa Madrid na walifanikiwa tatizo likawa kuweka mpira kwenye nyavu: kipindi cha kwanza Chelsea walipata nafasi nyingi wakakosa Ufanisi mbele ya lango. Chelsea wasipokuwa na mpira mda mwingi walipress na wachezaji wanne kuanzia juu.


Madrid walilenga kushambulia kwa kushtukiza , wakati wakipora mipira wanakuwa sharp sana kuunda mashambulizi (Vin Jr & Rodrygo) walikuwa pembeni zaidi ya uwanja , wakitumia space nyuma ya mawingbacks na walifanikiwa + long balls kwenda pembeni “Just Wow”👏🏻


✍🏻 Chelsea kwa zile chance kipindi cha kwanza 🤔 wanahitaji mshambuliaji.


✍🏻 Rodrygo “Finisher✅” anahitaji nafasi moja tu! Akuadhibu🙌


✍🏻 Kante “What a perfomance” ameubonda sana👏🏻 ile Lampard akiangalia kwenye benchi alafu kwa nafasi anazopata mh🤔


✍🏻 Modric , Kross na Valverde wakiwa na mali mguuni🙌 asee utulivu mkubwa mno👏🏻 Thibat Courtois 🙌


FT: Chelsea 0-2 Real Madrid (Agg 0-4)

Comments

Popular posts from this blog

PACHA HATARI