SALIBA HACHEZI GAME YA MAN CITY
.
Ishakuwa soo. Arsenal inakabiliwa na pigo kubwa baada ya kuripotiwa kwamba beki wao William Saliba hatakuwapo kwenye mechi muhimu kabisa ya kutambua hatima yao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City.
.
Arsenal watakabiliana na wapinzani wao kwenye mbio hizo za ubingwa, Aprili 26 uwanjani Etihad. Kwa mujibu wa Evening Standard Arsenal watakabiliana na Man City Ijumaa bila ya huduma ya Saliba. Mchezaji huyo bado hajapona vyema majeruhi yake aliyopata kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Sporting Lisbon.

Comments
Post a Comment