ROBERTINHO AMEANZA KUELEWEKA
ROBERTINHO MMEMUELEWA SASA
Sasa mashabiki wa Simba wanamuelewa kocha wao mbarizil, Robert Olivieira 'Robertinho'. Hiyo ni baada ya mechi tatu kubwa na ngumu mfululizo.
Robertinho aliuendea vema mchezo wa ligi dhidi ya Yanga, akafanikiwa kuwapa Simba ushindi wa kwanza wa ligi mbele ya Yanga baada ya miaka minne.
Mechi mbili za robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca, Robertinho amezicheza tena vema japo ametupwa nje lakini Simba wamemuelewa kocha wao.
Unakumbuka Robertinho alivoanza kazi Simba? Mashabiki wa Simba walimchukia mara moja na wengi tulidhani hatafika mwezi wa nne kucheza dhidi ya Yanga.
Ni kipindi kile ambacho alikuwa na ujasiri wa kumtoa Clatous Chama katika dakika za mapema kwa kuamini kwamba Chama hafanyi sawa na mpango wake.
Lakini ni kipindi hichohicho ambacho alikuwa anampanga Denis Kibu takribani kila mechi na mashabiki wa Simba walikuwa hawapendi anachokifanya kocha.
Lakini sasa wanamuelewa. Kumbe lilikuwa ni suala la muda tu kabla alichokuwa anakifundisha hakijaeleweka na kumvutia kila mmoja.
Robertinho anaonekana kuwa kocha mzuri wa mbinu na mtu mwenye misimamo kwa kile anachokiamini. Makocha wakubwa wana tabia hii.
Tujifunze kuwaelewa wachezaji na makocha mwanzoni.

Comments
Post a Comment