BUKAYO SAKA AOMBA RADHI .
.
Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka amewaomba radhi mashabiki baada kukosa penalti muhimu katika sare ya mabao 2-2, dhidi ya West Ham.
.
Baada ya mchezo kumalizika Saka akawaomba radhi mashabiki wa Arsenal kupitia akaunti yake ya Twitter kutokana na makosa yake.
.
“Kutokana na kilichotokea, siku zote nabeba majukumu, haijalishi nini kitatokea, nawaomba radhi mashabiki wa Arsenal, nitafanya juu chini kuweka mambo sawa,” aliandika Saka.
.
Huo ulikuwa mchezo wa pili mfululizo ambao washika bunduki wanadondosha pointi na kupunguza pengo la pointi kufikia nne dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola wakiwa na mchezo mkononi.
…………

Comments
Post a Comment